Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 129 KUMTEGEMEA MWOKOZI nyimbo za wokovu
1
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni.
Yesu, Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti,
Yesu, Yesu yu thamani,
Ahadi zake kweli.
2
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.
3
Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kwake daima Napata,
Uzima na amani.
4
Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu, M-Pendwa, Rafiki,
Uwe nami dawamu.