Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 127 NI SALAMA ROHONI MWANGU nyimbo za wokovu
1
Nionapo amani kama shwari,
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.
2
Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani,
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.
3
Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Huwekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.
4
Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.