Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 119 ALILIPA BEI nyimbo za wokovu
1
Yesu anasema,
Wewe huna nguvu
Kesha ukaombe,
Nauje, Mwanangu
Alilipa bei,
Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa,
Aliiondoa
2
Bwana nimeona
Uwezo wako tu
Waweza ‘takasa
Mioyo michafu
3
Sina kitu chema
Kudai neema,
Hivi nitafua
Mavazi kwa damu.
4
Ninaposimama
Juu ya mawingu,
Taji nitaweka
Miguuni pa Yesu.