Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 112 WEWE UMECHOKA SANA? nyimbo za wokovu
1
Wewe umechoka sana?
Wataka raha?
Kwake Yesu utapata –
Msaada.
2
Alama anazo Yeye?
Sana! Makovu
Ya mikono, na miguu,
Na mbavu.
3
Naye amevikwa taji
Kichwani Mwake?
Taji, kweli, alivikwa –
Miiba!
4
Huku nikimfuata,
Nipate nini?
Maonjo nje, na ndani –
Amani.
5
Kwamba namwandama Yeye,
Mwisho ni nini?
Kurithi furaha naye –
Milele.