Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 108 TUMESIKIA MBIU nyimbo za wokovu
1
Tumeisikia mbiu;
Yesu huokoa;
Utangazeni kote,
Yesu huokoa.
Tiini amri hiyo;
Nchini baharini.
Enezeni mbiu hii;
Yesu huokoa.
2
Imba nawe askari;
Yesu huokoa ;
Kwa nguvu ya kombozi,
Yesu huokoa.
Imbeni wenyewe shida,
Unapoumwa moyo,
Na kaburini imba;
Yesu huokoa.
3
Mawimbini uenee,
Yesu huokoa;
Wenye dhambi jueni;
Yesu huokoa;
Visiwa na viimbe,
Vilindi itikeni,
Na nchi shangilie;
Yesu huokoa.
4
Upepo utangaze,
Yesu huokoa;
Mataifa yashangaa,
Yesu huokoa;
Milimani, bondeni,
Sauti isikike
Ya wimbo wa washindi;
Yesu huokoa.