Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 100 KUWATAFUTA WASIOWEZA nyimbo za wokovu
1
Kuwatafuta wasioweza,
kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake
Njooni kwangu, nawapenda.
Nitakwenda
(Nitakwenda) niwatafute
Wapotevu
(Wapotevu) wageuke,
Waingie
(Waingie) katika zizi
La Mwokozi
(La Mwokozi) Yesu Kristo.
2
Kuwatafuta wasioweza,
waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote
uzima ule wa milele.
3
Kazi hiyo nataka kufanya,
leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao,
waletwe kwake Yesu Njia.