Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 1 MTAKATIFU, MTAKATIFU nyimbo za wokovu
1
U Mtakatifu Mungu mwenyezi,
Alfajiri sifa zako tutaimba,
U Mtakatifu Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote, Hata milele.
2
U Mtakatifu na Malaika,
Wengi sana wanakuabudu wote,
Elfu na maelfu wanakusujudu,
Wa zamani na, Hata milele.
3
U Mtakatifu ingawa giza,
La kuficha fahari tusiione,
U Mtakatifu Wewe peke yako,
Kamili kwa-u, Wezo na pendo.