Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 81 SIKU SITA ZIMEPITA nyimbo za wokovu
1
Siku sita zimepita,
Sabato tena karudi;
Shangilie roho yangu,
itukuze kwa busara.
2
Msifuni awapaye
pumziko tamu wachovu,
Kwake roho yatulizwa,
kupita siku nyingine.
3
Moyo wetu ufurahi,
na kuto mashukuru;
Ujalizwe raha ile,
yasiyopitika kamwe.
4
Raha hiyo ya rohoni,
ni amana ya pumziko
Ambalo limewekwa juu,
kikomo cha masumbuko.