Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 75 MSINGI IMARA, NANYI WA BWANA nyimbo za wokovu
1
Msingi imara,
Ninyi wa Bwana,
Umewekwa kwenu
Kwa neno lake.
Nini zaidi
Atasema Bwana,
Imani yenu
Ipate kuzidi?
2
Wambiwapo vuka
Maji ya giza,
Mito ya mashaka
Haitazidi;
‘Tukuwapo nawe,
Nikuwezeshe,
Shida upatazo
Zisikutishe!
3
Utakapopishwa
Ndani ya moto,
Nguvu nitakupa,
Upate pato;
Huteketezwi,
Ila taka zako.
Na zitasalia
Dhahabu zako.
4
Na mtu aliyenitegemea
Nguvu za Jehanamu
Zijapotisha,
Kamwe kwa adui
Sitamtia;
Mtu wangu kamwe
Sitamuacha.