Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 44 URAFIKI WA YESU nyimbo za wokovu
1
Hakuna rafiki kama Yesu,
Hakuna, hakuna!
Tabibu mwingine wa rohoni,
Hakuna, hakuna!
Yesu ajua shida zetu;
Daima ataongoza,
Hakuna rafiki kama yesu,
Hakuna hakuna;
2
Wakati ambapo hapo yeye,
Hapana, hapana!
Wala giza kututenga naye,
Hapana, hapana!
3
Aliyesahauliwa naye,
Hakuna, hakuna!
Mkosaji asiyempenda,
Hakuna, hakuna!
4
Kipawa kama Mwokozi wetu,
Hakuna, hakuna!
Ambaye atanyimwa wokovu,
Hakuna hakuna!