Nyimbo za wokovu
Wimbo 137 Aligusa Upindo Wa Nguo Maneno ya wimbo
Aligusa upindo wa nguo
Ya Yesu safarini.
Mara akaona amepzwa Humo makundini.
Uguse upindo wake,
Nawe utapoa.
Ni sasa saa ya kufaa,
Atakuokoa.
Akamwendea akitetemeka,
Na hofu moyoni,
Akasikia uwezo wake Mamwenea ndani.
Akasema Yesu, Binti sasa,
Enda na amani,
Ujue lililokutakasa
Ni yako imani.