Nyimbo za wokovu
Wimbo 130 Kwa Mizigo Yako Ukichoka Maneno ya wimbo
Kwa mizigo yako ukichoka,
Yesu aingie moyo;
Ukitamani kuishi upya,
Yesu, aingie moyo.
Sasa ondoa shaka,
Usimkatae tena;
Umkaribishe sasa,
Yesu aingie moyo.
Ukililia utakatifu,
Yesu aingie moyo;
Kisima cha damu ki karibu,
Yesu aingie moyo.
Ukiachwa na rafiki zako,
Yesu aingie moyo;
Hatakuacha na shida zako,
Yesu aingie moyo.
Kukaa naye ukitamani.
Yesu aingie moyo;
Ukipenda kufika mbinguni,
Yesu aingie moyo.