Nyimbo za wokovu
Wimbo 18 Ukirushwa-rushwa Na Dunia Hii Maneno ya wimbo
Ukirushwa-rushwa na dunia hii,
Utakapokufa moyo kwa kudhii,
Zilizo baraka zihesabu tu,
Nawe utaona ni ajabu kuu.
Zilizobaraka zihesabu tu,
Mungu aliyofanya ndio makuu,
Zilizobaraka zihesabu tu
Nawe utaona ni ajabu kuu.
Je, unalemewa na mzigo huu,
Msalaba wako ni uzito tu?
Hesabu baraka, za chini na juu,
Hazinunuliki kwa thamani kuu.
Yatuumizayo tutayasahau,
Na baraka zetu tusizidharau,
Hesabu baraka, zisipotee,
Hesabu baraka, hata uzoee.
Haya basi ndugu, twende mbele tu,
Na tusife moyo, Mungu ni mkuu,
Hesabu baraka, nawe mngojee,
Hata mwisho atakuwa na wewe.