Nyimbo za wokovu
Wimbo 13 Na Tumwabudu Huyo Mfalme Maneno ya wimbo
Na tumwabudu huyo Mfalme,
Sifa za nguvu zake zivume;
Ni ngao, ni ngome, Yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.
Hubirini ya uweza wake,
Mkaimbie neema yake;
Gri yake ndiyo mawingu, nayo
Ni nuru mavao ayavaayo.
Tazameni ulimwengu huu,
ulivyoumbwa, ajabu kuu,
Sasa umewekwa mahali pake,
Hata utimize majira yake.
Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana,
Twakushukuru, U mwema sana;
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kina mahali pake.
Wanadamu tu wanyonge sana,
Twakutumaini Wewe, Bwana;
Kamwe haipungui wako wema,
Mkombozi wetu, Rafiki mwema.
Uweza wako haupimiki;
Mapenzi yako hayasemeki;
Na ulivyoumba vyote kabisa
Vidogo, Vikubwa, vyakutukuza.