Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 192 MWAMBA WENYE IMARA nyimbo za wokovu
1
Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha!
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.
2
Kwa kazi zote pia
Sitimizi sheria.
Nijapofanya bidii,
Nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa;
Ndiwe wa kuokoa.
3
Sina cha mkononi,
Naja msalabani;
Nili tupu, nivike;
Ni mnyonge, nishike
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.
4
Nikungojapo chini,
Na kwenda kaburini;
Nipaapo mbinguni,
Na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe.