Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 190 RAHA YANGU YOTE, BWANA nyimbo za wokovu
1
Raha yangu yote, Bwana,
I mbavuni pako;
Mimi sina haja tena
ila kifo chako;
2
Mwokozi uliyekufa,
nawe ndiwe Mungu,
Kifo chako ni kwa dhambi,
ziondoe zangu.
3
Nioshe na niwe wako,
nawe uwe wangu;
Nioshe damuni mwako
liwe fungu langu.
4
Nioshe si miguu tu,
osha tangu nyayo,
Hata kichwa changu juu,
na ndani ya moyo.
5
Na iwe kafara damu
nifanyapo kazi,
Hata imani itimu,
nikwone, Mwokozi.