Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 172 MFALME AJAPO nyimbo za wokovu
1
Mfalme wetu atuita
Tukae karamuni Kwake;
Itakuwaje nasi kule
Bwana ajapo?
Bwana ajapo, ndugu,
Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi,
Bwana akija?
2
Atavikwa vizuri sana,
Taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari
Bwana ajapo.
3
Kwa furaha awakubali
Wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha
Bwana ajapo.
4
Kutakuwako na utengo;
Watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile
Kristo ajapo.
5
Mfalme utupe neema
sisi tunapokungojea,
Tusiogope kukuona
Ujapo Bwana.