Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 171 HUKUMU IMEANZISHWA nyimbo za wokovu
1
Imeanzishwa hukumu mbinguni;
Tutasimamaje pale
Apimapo Mungu Hakimu
Kila wazo na tendo?
Tutasimamaje sote
katika siku kuu ile?
Dhambi zetu zitafutika
ama zitatuangusha?
2
Wametangulia wafu kupimwa,
Kitambo ndipo Wahai,
Watapokea neno la mwisho,
Vitabuni mwa Mungu.
3
Tutasimamaje usiku ule,
Siri zetu, kila moja,
Zafunuliwa toka vitabu;
Yesu atusaidie!