Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 146 TWAE WANGU UZIMA nyimbo za wokovu
1
Twae wangu uzima,
Sadaka ya daima;
Twae saa na usiku
Zikutukuze huku.
2
Twae mikono, nayo
Ifanye Upendayo,
Twae yangu miguu,
Kwa wongozi wako tu.
3
Twae sauti yangu,
Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo,
Ijae neno lako.
4
Twae dhahabu pia
Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima
Upendavyo tumia.
5
Nia itwae, Mungu
Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako,
Uwe makazi yako
6
Twae mapenzi yangu,
Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi
Niwe wako halisi.