Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 130 YESU KWETU NI RAFIKI nyimbo za wokovu
1
Yesu kwetu ni Rafiki,
Hwambiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye,
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kama tulimwomba Mungu;
Dua alisikia.
2
Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema,
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.
3
Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa,
Ujaporushwa pia.
Watu wakikudharau,
Wapendao dunia,
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.