Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 121 KATIKA WENYE DHAMBI nyimbo za wokovu
1
Katika wenye dhambi
Ndimi mkuu wao
Ila Yesu akaja,
Kwa dhambi alikufa,
Akamimina damu
Niupate uzima.
2
Ajabu! Pendo lake!
Pendo lililo kuu,
Pendo lisilo mwisho,
Lidumulo milele-
Lililonitafuta
Ingawa sikumpenda.
3
Ingawa ni mbaya
Kristo ni vyote kwangu;
Ajua haja zangu;
Huzuni zangu, zake;
Hata katika vita,
Akiwapo Salama.