Nyimbo za wokovu
Wimbo 94 Kristo Ametukomboa Maneno ya wimbo
Kristo ametukomboa,
Mwokozi wa ajabu;
Deni zetu zililipwa
Naye Mwokozi wangu.
Mwokozi wa ajabu,
Yesu, ndiye Yesu;
Mwokozi wa ajabu,
Ndiye Bwana wangu.
Kwa damu nimesafishwa,
Mwokozi wa ajabu;
Kwa hiyo napatanishwa,
Mwokozi wa ajabu.
Ndani yangu anakaa,
Mwokozi wa ajabu;
Niwe mnyofu wa kufaa,
Mwokozi wa ajabu.