Nyimbo za wokovu
Wimbo 90 Ahadi Ya Bwana Maneno ya wimbo
Ahadi ya Bwana tuingojea,
Kutoka mbingu itatujalia
Kwa imani yetu twaipokea,
Kungoja orofani.
Uwezo!
Uwezo!
Hutupa ushindi
Na usafi ndani;
Uwezo!
Uwezo!
Uwezo wa Pentekoste.
Kwake Bwana Yesu tutamtolea,
Kutoka dhambi atatufungua;
Pumzi ya uzima tutaipata,
Kungoja orofani.
Twatamani kuendelea mbele,
Kumngojea Bwana tupate tele;
Moto wa Mbingu na ututakase,
Kungoja orofani.