Nyimbo za wokovu
Wimbo 85 Na Pentekoste Ya Kale Maneno ya wimbo
Na Pentekoste ya kale,
Watu walijazwa;
Moto wako ulishuka,
Leo twautaka.
Bwana, utujalie
Na nguvu zako tele,
Baraka za kale utufungulie;
Bwana utujalie
Na nguvu zako tele,
Waovu waokoke na tuimbe shangwe.
Kazi na itayarishwe,
Kwako itendeke:
Bwana utuimarishe,
Na tusianguke.
Ziharibu dhambi zote,
Na utujalie;
Tufanye kazi na bidii,
Kwako kwa milele.
Useme nasi Ee, Bwana,
Tukikungojea;
Hatutakuacha hata
Tupewe baraka.