Nyimbo za wokovu
Wimbo 78 Aniongozapo Pote Maneno ya wimbo
Aniongoza popote,
Nimwandame siku zote;
Kwaajili yangu mimi,
Aliuawa kalvari.
Nitaongozwa na Bwana,
Usiku kucha na mchana;
Yesu rafiki wa heri,
Ninakumbuka kalvari.
Lanitosha neno lake,
Nishikwe na mkono wake;
Mapenzi yake ni heri,
Yalitimizwa kalvari.
Nitaendelea mbele,
Pamoja naye milele;
Pendo lake ni hiari,
Bwana Yesu kwa Kalvari.