Nyimbo za wokovu
Wimbo 75 Nikimaliza Kazi Ya Maishani Maneno ya wimbo
Nikimaliza kazi ya maishani mwangu,
Nitaacha dunia kwa salama;
Nitamjua Mwokozi, nikifika huko juu,
Atanikaribisha kwa furaha.
Nitamjua, nitamjua,
Nikisimama karibu kwake;
Nitamjua, nitamjua,
Kwa makovu mikononi mwake.
Mle mbinguni nitamshangilia Mwokozi,
Nikimwona Yesu uso kwa uso;
Amestahili sifa, aliye Mkombozi,
Amenipa rehema na upendo.
Nitaona wale walionitangulia,
Waniashiria niende pale;
Nitafurahi nao nitakapoingia,
Bali mwanzoni, Mwokozi nimwone.
Nikifika nitaivikwa mavazi meupe,
Sitaona huzuni pale, kamwe;
Kwa furaha nitaimba wimbo wa milele,
Bali mwanzoni, Mwokozi nimwone.