Nyimbo za wokovu
Wimbo 7 Jina Lake Yesu Tamu Maneno ya wimbo
Jina lake yesu tamu.
Tukilisikia,
Hutupoza tena hamu,
Hutuondolea.
Roho iliyoumia,
Kwalo hutibika,
Chakula njaani pia;
Raha, tukichoka.
Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi,
Kwangu ni akiba.
Yesu, Mchunga, Rafiki,
Mwalimu, kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.
Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.
Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha,
Kukusifu sana.