Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 58 Yesu, Msalaba Wangu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 58 Yesu, Msalaba Wangu Maneno ya wimbo

 

Yesu, msalaba wangu
Sasa nimejitweka,
Nikwandame Bwana wangu,
Wengine kuepuka.
Sina tamaa ya mali,
Mali ya ulimwengu;
Mimi ni tajiri kweli,
Ni mrithi wa Mungu.

Wajaponisumbuaje,
Nitakukimbilia;
Mashaka yote na yaje,
Nitayavumilia.
Taabu hazinidhuru,
Nina mapenzi yako;
Na kwa haya nashukuru,
Napata yote kwako.

Moyo, pokea wokovu,
Kila siku wokoke;
Ushinde dhambi na hofu;
Subiri, utumike;
Roho yuko ndani yako,
Una pendo za Baba,
Mwokozi naye ni wako;
Mwenye hivyo, si haba.

Hima nawe kaza mwend:
Ujivike imani;
Hujafika mbingu bado,
Kwa Mungu tumaini:
Mwisho wa safari yako
Wasongea upesi;
Utakapofika huko,
Ni furaha halisi.

Exit mobile version