Nyimbo za wokovu
Wimbo 48 Enyi Askari wa Kristo Maneno ya wimbo
Enyi askari wa Kristo,
Mlio vitani;
Mwe hodari kwa bidii,
Msishindwe kweli.
Adui zetu washindwe
Na nguvu za Yesu,
Imani ni nguvu zetu,
Hushinda uovu.
Imani ni nguvu,
Imani ni nguvu;
Nguvu za utukufu,
Hushinda uovu.
Bendera yake ni pendo,
Upanga ni Neno;
Tuishike njia yetu,
Tufanye vifijo:
Watakatifu wa kale
Wakawa washindi,
Kwa imani ishindayo
Tushinde vitani.
Ashindaye atapewa
Mavazi meupe,
Malaika watamjua
Akatajwa mle;
Tuendelee na pendo
Majeshi tushinde,
KatikaJina la Yesu
Tuishi milele.