Nyimbo za wokovu
Wimbo 32 Useme Nami Bwana Maneno ya wimbo
Useme nami Bwana, uninong`oneze,
Useme na upendo kwamba sitaachwa;
Uufungue moyo ili nisikie,
Unijaze na sifa nikushangilie.
Useme nami Bwana, useme na pendo,
Nitakua mshindi kwa uweza wako;
Useme kila siku, nitakusikia,
Useme nami Bwana, kwamba sitaachwa.
Useme nasi Bwana, kwkao tuongozwe,
Tujazwe na furaha na utufundishe;
Tujitoe uzima kwa Ufalme wako,
Mbinguni kwa Milele, tukuone humo.
Kama ulivyosema na watu wa kale,
Useme nasi sasa, Neno litendeke;
Utukuzwe Bwana, siku zangu zote,
Nikuheshimu pia, sasa na milele.