Nyimbo za wokovu
Wimbo 25 Yesu Uniongoze Maneno ya wimbo
Yesu uniongoze,
Juu ya bahari yote;
Nisizame majini,
Dira yako nipate,
Yesu uniongoze.
Kwa bahari waweza,
Maji yake kushinda;
Mawimbi yasikia
Usemapo, Tulia;
Bwana wa bahari Ewe,
Yesu, uniongoze.
Nifikapo ardhini
Kwa kuvuka kilindi,
Nitapata pumziko
Kutegema kwako;
Uniambie tena,
Ndiyo, Nitaongoza.