Nyimbo za wokovu
Wimbo 204 Bwana Yangu Yu Mchungaji Maneno ya wimbo
Bwana wangu yu mchungaji,
Hunilaza chini;
Kwa malisho ya majani
Huniongoza mimi.
Nafsi yangu huhuisha,
Ananitembeza
Njiani mwake kwa haki yake,
Katika jina lake.
Nijapopita bondeni
Mwisho mwa maisha,
Sitaogopa baya lo lote,
Wewe upo na mimi.
Wema wako na fadhili,
Itanifuata
Katika nyumba yake Mungu,
Kutakuwa makao.