Nyimbo za wokovu
Wimbo 203 Nikilemewa Na Mizigo Mingi Maneno ya wimbo
Nikilemewa na mizigo mingi,
Nikitembea bila tumaini;
Mwokozi wangu ameniahidi,
Niambie ahadi zake tena.
Niimbie ahadi tena,
Mara kwa mara ahadi tena;
Na nitafurahi, hapana huzuni,
Niambie ahadi zake tena.
Nikizungukwa na hatari nyingi,
Na nikishikwa na hofu moyoni;
Sitakuacha, asema Mwokozi,
Niambie ahadi zake tena.
Na nikiingia mbinguni kwake,
Kupumzika salamani milele;
Ahadi zake tamu, zikumbukwe,
Niambie ahadi zake tena.