Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 195 Mnona Humkubali Mwokozi Sasa Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 195 Mnona Humkubali Mwokozi Sasa Maneno ya wimbo

 

Mbona humkubali Mwokozi sasa?
Kwa upole akusihi;
Umjie Yesu, anakungojea,
Kusamehe Yu tayari.

Mbona humkubali?
Mbona? Mbona?
Usimkatae anakusihi,
Umkubali sasa.

Roho hatakusihi siku zote,
Umkubali Yesu sasa;
Labda kesho hutapata nafasi,
Usichelewe kabisa.

Twae Kristo awe Mwokozi wako,
Utakuwa na salama;
Mambo ya kesho yajapokujia,
Hutaogopa mashaka.

Exit mobile version