Nyimbo za wokovu
Wimbo 188 Nifanye Nini Niokolewe Maneno ya wimbo
Nifanye nini niokolewe?
Mlinzi akauliza;
Paulo akamjibu akisema,
Mwamini Yesu Bwana.
Umwamini Bwana Yesu,
Umwamini Bwana Yesu;
Umwamini Bwana Yesu,
Utaokoka.
Nifanye nini? Usiogope,
Umkimbilie Bwana;
Atakukubali kwa samaha,
Nawe utaokoka.
Damu yake imefaa sana,
Utakaso wa sifa;
Uje kupokea Bwana sasa,
Wokovu utapata.