Nyimbo za wokovu
Wimbo 185 Ati Twonane Mtoni Maneno ya wimbo
Ati twonane mtoni?
Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani,
Penye kiti cha Mungu.
Naam, twonane mtoni!
Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutana mtoni Penye kiti cha Mungu.
Tukitembea mtoni
Na Yesu Mchunga wetu;
Daima tu ibadani
Usoni pake kwetu.
Tukisafiri mtoni
Tutue ulemeao
Wema nda Mungu yakini:
Una taji na vao!