Nyimbo za wokovu
Wimbo 177 Mwokozi Wangu Alinifia Maneno ya wimbo
Mwokozi wangu alinifia,
Mbona anipenda?
Kwa msalaba aliniendea,
Mbona anipenda?
Mbona anipenda?
Mbona anipenda?
Mbona Mwokozi alijitoa?
Mbona anipenda?
Kwa dhambi zangu akafa mtini,
Mbona anipenda?
Ili nipate kwenda mbinguni,
Mbona anipenda?
Alichukua mahali pangu,
Mbona anipenda?
akaziondoa dhambi zangu,
Mbona anipenda?