Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 167 Kibarikiwa Kifungo Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 167 Kibarikiwa Kifungo Maneno ya wimbo

 

Kibarikiwe kifungo
Kitufungiacho mioyo,
Ushirika wetu wa fikira zetu
Ni kama ule wa mbingu.

Mbele ya enzi ya Baba,
Dua zetu twaziomba;
Hofu zetu na matumaini yetu,
Hayo ni mamoja kwetu.

Huzuni zetu twashika,
Na mizigo yetu pia;
Ndani yao yote twashirikiana
Hata katika kulia.

Tutawanyikapo mbali,
Hiyo yatufadhisha;
Lakini tungali pamoja rohoni
Hata tutakutanika.

Exit mobile version