Nyimbo za wokovu
Wimbo 16 Tunakusifu, Ewe Mungu Wetu Maneno ya wimbo
Tunakusifu, Ewe Mungu wetu,
Kwa Yesu mpendwa Mwokozi wetu.
Aleluya atukuzwe,
Aleluya Amin,
Aleluya utukuzwe,
Utufufue.
Tunakusifu, Roho Mtakatifu,
Uliondoa giza tuone nuru.
Tunakusifu, Kondoo wa dhabihu,
Ulichukua dhambi tupate huru.
Tunakusifu, kwa neema yako,
Uliyetutafuta tukae kwako.
Utufufue, tena utujaze,
Ili upendo wako utuendeshe.