Nyimbo za wokovu
Wimbo 158 Mle Kaburini Maneno ya wimbo
Mle kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa chini, Bwana wangu!
Bwana amefufuka,
Kifo kimeshindwa kabisa!
Gizani mle alitoka chini,
Sasa atawala huko mbinguni!
Yu hai!
Yu hai!
Bwana Yesu yu hai!
Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana ujao, Bwana wangu!
Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure ni muhuri, Bwna wangu!
Kifo kimeshindwa, Yesu Mwokozi!
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu!