Nyimbo za wokovu
Wimbo 144 Baragumu Yake Bwana Maneno ya wimbo
Baragumu yake Bwana wakati ikipigwa,
Na siku ya milele ikafika;
Hapo waliokombolewa watakusanyika,
Nitakuwako, jina kuitika.
Na majina yaitwapo,
Na majina yaitwapo;
Na majina yaitwapo,
Kuitika jina, nitakuwapo.
Wafu wa Kristo wafufukapo kwa siku ile,
Tutashiriki na fahari yake;
Waliochaguliwa watakaribishwa kwake,
Nitakuwapo jina kuitika.
Saa zote na tumfanyie Bwana kazi yake,
Tangu asubuhi hata jioni;
Maisha yetu ikomapo humu duniani,
Nitakuwako jina kuitika.