Nyimbo za wokovu
Wimbo 133 Nimetembelea Mbali Maneno ya wimbo
Nimetembelea mbali,
Sasa narudi;
Nilipotea dhambini,
Sasa narudi.
Narudi, narudi,
Kutoka mbali;
Sasa unikaribishe,
Bwana, narudi.
Nimepoteza miaka mingi,
Sasa narudi;
Tena nazitubu dhambi,
Sasa narudi.
Nimechoka na dhambi, Bwana,
Sasa narudi
Neno lako naamini,
Sasa narudi.
Nimevunjika, siwezi,
Sasa narudi;
Nipate nguvu na amani,
Sasa narudi.