Nyimbo za wokovu
Wimbo 124 Uje Kutoka Dhambini Maneno ya wimbo
Uje kutoka dhambini,
Jifiche damuni mwa Yesu;
Uje atakukubali,
Damuni mwa Yesu
Jifiche damuni
Ukiona hatari,
Jifiche damuni,
Ukiona hatari.
Uje kwake kwa Salama,
Jifiche damuni mwa Yesu;
Uje kupata uzima,
Jifiche damuni mwa Yesu.
Uje kupata msamaha,
Jifiche damuni mwa Yesu;
Uje kuona furaha,
Jifiche damuni mwa Yesu.