Nyimbo za wokovu
Wimbo 101 Nilitembea Mbali Maneno ya wimbo
Nilitembea mbali katika dhambini,
Nikapoteza hali nikashuka chini;
Kwake Mwokozi Bwana, nikamlilia,
Akanishika sana kuokoa.
Na upendo, na upendo,
Nimeinuliwa sana na upendo;
Na upendo, na upendo,
Nimeinuliwa sana na upendo.
Moyo wangu nampa, nitamshika pia,
Nitakaa na Yesu, sifa kumwimbia;
Upendo wa hakika wastahili sifa,
Na uaminifu ni wake pia.
Mliomo shidani, tazameni Bwana,
Atawaponya kweli, kutoka mashaka;
Atawasimamisha na upendo wake,
Awe Mwokozi kwa wokovu wake.