Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 96 Kazi Yangu lkiisha. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 96 Kazi Yangu lkiisha. Maneno ya wimbo

 

Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka
Na kuvaa kutokuharibika
Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki

Chorus
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari

Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliyoyatuandalia
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni

Nao waliokufa katika BwanaYesu
Nitawaona tena huko juu
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni
Nataka kumwona Mwokozi kwanza

Milangoni mwa mji Bwana atanipisha
Pasipo machozi wala huzuni
Nitauimba wimbo wa milele, lakini
Nataka kumwona mwokozi kwanza

Exit mobile version