Nyimbo Za Sifa
Wimbo 88 Nataka Nimjue Yesu. Maneno ya wimbo
Nataka nimjueYesu
Na nizidi kumfahamu
Nijue pendo lake, na
Wokovu wake kamili
Chorus
Zaidi, zaidi nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake, na
Wokovu wake kamili
Nataka nioneYesu
Na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni
Kujidhihirisha kwangu
Nataka nifahamu, na
Nizidi kupambanua
Mapenzi yake, nifanye
Yale yanayompendeza
Nataka nikae naye
Kwa mazungumzo zaidi
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake