Nyimbo Za Sifa
Wimbo 7 Taji Mvikeni. Maneno ya wimbo
Taji Mvikeni
Taji nyingi tena,
Kondoo mwake Kitini
Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu
Alikufa kwangu,
Ni Mfalme mtukufu,
Mkuu wa Mbingu.
Taji mvukeni
Mwana wa bikira;
Anazovaa kichwani
Aliteka nyara;
Shiloh wa manabii,
Mchunga wa watu,
Shina na tanzu vya Yesu
Wa Bethilehemu.
Taji mvikeni
Bwana wa mapenzi;
jeraha zake ni shani
Ni vito vya enzi,
Mbinguni hakuna
Hata malaika
Awezaye kuziona
Pasipo kushangaa