Nyimbo Za Sifa
Wimbo 68 Twendeni Askari. Maneno ya wimbo
Twendeni askari, watu wa Mungu
Yesu yuko mbele tumwandame juu
Ametangulia Bwana vitani
Twende mbele kwani ndiye amini
Chorus
Twende askari watu wa Mungu
Yesu yuko mbele, tumwandame juu
Jeshi Ia Shetani, likisikia
jina Ia Mwokozi Iitakimbia
Kelele za shangwe zivume nchini
Ndugu inueni zenu sauti
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu
Sisi na mababa tu moja
Hatutengiwi nao, moja imani
Tumaini moja, na moja dini
Haya mbele watu nasi njiani
lnueni myoyo, nanyi sifuni
Heshima na sifa ni ya Mfalme
juu hata chini, sana zivume