Nyimbo Za Sifa
Wimbo 61 Ndugu wa Kirohoni. Maneno ya wimbo
Ndugu wa kirohoni
Mliokombolewa
Tafakarini sana
Yatupasayo
Chorus
Wapenzi wake Yesu
Tuliokombolewa
Tujitoe kabisa
Wengi waponywe
Siku itatimia
Tutakapoulizwa
Wale wa nyumba zetu
Na majirani
Tujitoeni, ndugu
Tukahubiri Iniili
Atutumie Roho
Kuponya wengi
Wasiokombolewa
Ni wengi vijijini
Wataokolewaje
Tukiogopa?
Bwana alijitoa
Akapotewa mengi
lli atuokoe
Tusiwe waoga
Aliyetununua
Kwa kuimwaga damu
Angalieni sana
Msimwepuke