Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 6 Ni Tabibu wa Karibu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 6 Ni Tabibu wa Karibu. Maneno ya wimbo

 

Ni taibu wa karibu;
Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima;
Ni dawa yake njema

Chorus
Imbeni, malaika
Sifa za Yesu Bwana
Pweke limetukuka
jina lake Yesu

Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai,
llaYeye kweli ndiye
Atupumzishaye.

Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twenendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.

Huliona tamu jina
LaYesu Kristo Bwana
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa

Kila mume asimame
Sifa zake zivume
Wanawake na washike
Kusifu jina Iake

Na vijana wote tena,
Wampendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake

Exit mobile version